Aaron Ally(Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa All-stars Students Awards
Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake(Ms Chiku Lweno, Mwalimu Mtanga)
Dany Mtanga) wameanzisha Tuzo walizoziita All-stars Students
Awards. Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari
A-level na O-level za Afrika Mashariki.
Alhamisi hii Dj Aaron
alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV kuongelea tuzo
hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.
Aaron amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa
shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi
watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. pia na
walimu husika ambao ni chachu ya wanafuzi ambao wamefanya vizuri kwenye
hayo masomo.Tuzo hizo zitaaangalia namba moja wote waliongoza katika
nchi zote za Africa Mashariki. Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili,
Hesabu, Fizikia, Kemia, Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo
utaanza katikati ya mwezi wa sita.pia Special Talents, Michezo na
Shule bora